WAKA MEDIA

kwa habari za uhakika isiyochujwa

Rashford atunukiwa Udaktrari

1 min read

By Abraham Morogosho

NYOTA wa timu ya Manchester United, Marcus Rashford ametunukiwa udaktari wa heshima na Chuo Kikuu cha Manchester kutokana na harakati zake zinazopinga ubaguzi, umasikini na njaa kwa watoto.

Rashford 23, ameweka rekodi ya kuwa kijana mwenye umri mdogo kutunukiwa udaktari huku harakati zake zikiwa zinakubalika na viongozi wengi akiwemo aliyekuwa Rais wa Marekani, Barrack Obama.

Akizungumza mara baada ya kutunukiwa udaktari, Rashford alitumia nafasi hiyo kueleza jinsi anavyopambana kwa kushirikiana na Serikali ya Uingereza kuhakikisha wanawapatia chakula watoto wenye mazingira magumu.

Mamilioni ya familia hapa Uingereza yalipoteza mwelekeo wa maisha na upatikanaji  wa chakula, juhudi zimeonekana leo watato masikini wakisogea kwenda hatua nyingine, kwa sababu hiyo leo ni siku ya furaha kwangu,” amesema Dk Rashford.

Awali Rashford alipaswa kutunukiwa cheo hicho mwezi Julai mwaka jana, ila kutokana na tatizo la virusi vya corona, hafla hiyo ilisitishwa.

2 thoughts on “Rashford atunukiwa Udaktrari

Leave a Reply to Omary Cancel reply

Your email address will not be published.